Fahamu zaidi kuhusu Bulk SMS, Matumizi na Jinsi ya Kujisajili

Bulk SMS ni huduma inayowawezesha kutuma jumbe fupi kwa kundi kubwa la watu kwa wakati mmoja. Huduma hii ni muhimu sana kwa biashara, makanisa, shule, vyuo, na taasisi mbalimbali kwa kuwa inatoa njia rahisi ya kufikisha ujumbe kwa haraka na kwa ufanisi. Katika makala hii, tutajadili:

  1. Bulk SMS ni Nini? – Ufafanuzi wa huduma hii.
  2. Kwa Nini Bulk SMS ni Muhimu? – Sababu za kuwa na Bulk SMS.
  3. Jinsi Bulk SMS Inavyofanya Kazi – Mchakato wa kutuma SMS kwa wingi.
  4. Faida za Bulk SMS – Kwa makanisa, shule, vyuo, na biashara.
  5. Features za Mfumo Wetu wa Bulk SMS – Vipengele vya kipekee vinavyopatikana kwenye mfumo wetu.
  6. Kuhusu Sender ID – Maana na faida za Sender ID.
  7. Jinsi ya Kujiunga na Huduma ya Bulk SMS – Hatua za kuanza kutumia huduma yetu.

1. Bulk SMS ni Nini?

Bulk SMS ni huduma inayoruhusu kutuma jumbe fupi (SMS) kwa kundi kubwa la watu kwa wakati mmoja. Huduma hii hutolewa kupitia mfumo wa kidigitali wa Bulk SMS, na mtumiaji anahitaji kuwa na internet ili kutumia huduma hii. Hata hivyo, mpokeaji anapokea ujumbe huo kama SMS, bila kujali kama anatumia simu ya kitochi au smartphone.

2. Kwa Nini Bulk SMS ni Muhimu?

a) Matumizi ya Simu Yanaongezeka

Matumizi ya simu yanaongezeka kila siku, na takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya SMS bilioni 6 hutumwa kila siku duniani. Hii inathibitisha jinsi simu na SMS zilivyo muhimu kama njia ya mawasiliano.

b) SMS Husomwa kwa Haraka

Utafiti unaonesha kuwa 98% ya SMS hufunguliwa, na ujumbe huo husomwa ndani ya dakika 3 za kwanza. Hii inafanya SMS kuwa njia ya mawasiliano yenye ufanisi zaidi kuliko njia zingine kama vile email au matangazo ya televisheni na redio.

c) SMS Zinaweza Kupokelewa na Kila Mtu

SMS ni rahisi kumfikia mlengwa kirahisi, na zinapokelewa kwenye simu yoyote ile, iwe kitochi au smartphone, hivyo zinapatikana kwa wateja wengi zaidi.

3. Jinsi Bulk SMS Inavyofanya Kazi

Bulk SMS hufanya kazi kupitia jukwaa la mtandao ambalo linatumiwa kutuma ujumbe kwa watu wengi kwa wakati mmoja. Hii ni hatua kuu ya mchakato:

  • Kujiandikisha kwenye Mfumo: Mtumiaji anahitaji kuunda akaunti kwenye jukwaa la Bulk SMS.
  • Kuongeza Namba za Wapokeaji: Mtumiaji anaweza kuingiza namba za simu za wapokeaji kwa njia ya faili au kuzijaza moja kwa moja kwenye jukwaa.
  • Kuandika Ujumbe: Mtumiaji huandaa ujumbe wa SMS unaohitajika, kuhakikisha umeandikwa kwa lugha rahisi na yenye mvuto.
  • Kutuma na Kufuatilia Ujumbe: Baada ya kutuma, mtumiaji anaweza kupata ripoti ya ujumbe uliotumwa na kuona kama umefika kwa wapokeaji.

4. Faida za Bulk SMS

a) Faida kwa Makanisa

  • Kutuma matangazo ya ibada na mikutano.
  • Kuwajulisha washirika kuhusu matukio maalum kama harambee na semina.
  • Kukuza uhusiano kati ya viongozi wa dini na waumini kwa kuwapa taarifa muhimu kwa wakati.

b) Faida kwa Taasisi za Elimu (Shule na Vyuo)

  • Kuwasiliana na wazazi kuhusu maendeleo ya wanafunzi.
  • Kutuma ratiba za mitihani, matokeo, na taarifa za uandikishaji.
  • Kutoa taarifa za dharura kama likizo za ghafla au mabadiliko ya ratiba.

c) Faida kwa Biashara

  • Kutangaza ofa na bidhaa mpya kwa wateja wengi mara moja.
  • Kuwasiliana na wateja kuhusu huduma zao na kuwahamasisha kununua.
  • Kufanya kampeni za mauzo na kukuza chapa ya biashara kwa njia ya haraka.

5. Features (sifa) za Mfumo Wetu wa Bulk SMS

Mfumo wetu wa Bulk SMS una vipengele mbalimbali vinavyohakikisha utendaji bora na urahisi wa matumizi, ikiwa ni pamoja na:

  • Urahisi wa Kutuma Ujumbe: Inaruhusu kutuma jumbe kwa watu wengi kwa wakati mmoja.
  • Marekebisho ya Ujumbe: Unaweza kubinafsisha ujumbe na kuongeza sender ID yako.
  • Ripoti ya Kutuma Ujumbe: Unapata ripoti kamili kuhusu ujumbe uliotumwa na hali yake.
  • Usalama wa Taarifa: Mfumo wetu umejengwa kwa usalama, kuhakikisha taarifa zako zinakuwa salama.
  • Upatikanaji wa SMS Kimataifa: Unaweza kutuma ujumbe kimataifa kwa kutumia mfumo wetu.

6. Kuhusu Sender ID

Customize Your Sender ID With Your Company Name

1. Maana ya Sender ID:

  • Sender ID ni jina ambalo linaonekana kwenye sehemu ya “From:” katika ujumbe wa SMS. Ni kitambulisho kinachotumika kuonyesha ni nani anayepeleka ujumbe huo, na kinawawezesha wapokeaji kutambua chanzo cha ujumbe.

**2. Aina za Sender IDs:

  • Jina la Brand au Biashara: Hii ni kawaida kwa biashara au mashirika kutumia majina yao kama Sender ID (kwa mfano, “SAFARI LTD” kwa biashara yako).
  • Nambari za Telecommunication: Nambari maalum zinazotumika kutuma ujumbe kutoka kwa mtandao wa simu. (Mfano 177543)

**3. Faida za Sender ID:

  • Imani na Uaminifu: Sender ID inaunda uaminifu kwa wapokeaji kwani wanajua ni nani anayepeleka ujumbe.
  • Utambulisho wa Biashara: Inasaidia kuboresha utambulisho wa biashara yako na kufanya ujumbe wako kuwa wa kipekee na wa kitaalamu.
  • Kuboresha Mawasiliano: Inaleta ufanisi katika mawasiliano kati ya biashara na wateja au umma kwa ujumbe unaotoka kutoka kwa chanzo kilichojulikana.

**4. Masharti ya Sender ID:

  • Halipaswi kuzidi herufi 11 kwa urefu.
  • Herufi maalum zinapaswa kuepukwa, lakini alama za kuunganisha (-) na nukta (.) zinazoruhusiwa. Mfano M-TESA, M.TESA
  • Jina linapaswa kuhusiana na biashara au huduma yako unayotoa
  • Halipaswi kufanana na majina ya mashirika maarufu ili kuepuka kudanganya au kuiga chapa.

**5. Usajili na Idhini ya Sender ID:

  • Sender ID inahitaji uthibitisho na idhini kutoka kwa mtandao wa simu ili kuhakikisha kwamba haitumiki kwa madhumuni ya udanganyifu au kuiga kampuni au chapa nyingine. Kwa kuzingatia hili huwa tunatoa form ya maombi ya sender ID, nabayo utaambatanisha na taarifa/nyaraka za biashara yako.

**6. Muda wa Idhini:

  • Inachukua kati ya siku 5 hadi 14 za kazi kwa jina la mtumaji kuthibitishwa, kulingana na mtandao wa simu na nchi husika. Ila utakapojiunga nasi tutakupa sender id ya kuanzia , wakati unasubiri usajili wako wa id ukamilike,

7. Jinsi ya Kujiunga na Huduma ya Bulk SMS

Ikiwa unataka kuanza kutumia Bulk SMS, fuata hatua hizi rahisi:

  1. Fanya Malipo ya Kifurushi cha Kuanzia:

    Kifurushi cha kuanzia kinajumuisha SMS 1,000 na gharama ya Sender ID kwa mwaka mzima. Malipo ya kifurushi cha Starter Package ni Tsh. 34,600, ambayo inajumuisha:

    • Tsh. 15,000 kwa kifurushi cha SMS (ambapo tunachaji Tsh. 15 kwa SMS moja, hivyo utapata SMS 1,000).
    • Tsh. 19,600 kwa gharama ya Sender ID kwa mwaka mzima.

    LIPA KWA SIMU:

    • Mix by Yas: 8008206
    • M-Pesa: 5845779

    Jina litatokea: SDASMS

  2. Tuma Maelezo yako kwa Ajili ya Kufunguliwa Akaunti:

    Tuma jina lako kamili, barua pepe, na namba yako ya simu ili kufungua akaunti. Ikiwa ni taasisi, tuma taarifa za biashara yako (barua pepe, namba ya simu, na jina la taasisi).

    Tuma maelezo yako kwenda WhatsApp kwenye namba: 0658 600 302

  3. Kupokea Taarifa za Akaunti: Baada ya usajili, utapokea taarifa za akaunti yako pamoja na maelezo ya jinsi ya kutumia mfumo wetu.

Mawasiliano na Msaada zaidi.

Maswali yanayoulizwa zaidi som hapa