Jihusishe Kidijitali Kwa Kutumia Bulk SMS Kutangaza Injili.

Kuza, lea, hamasisha na shirikisha washiriki
kufanya kazi ya Mungu kwa njia ya SMS.

Gundua nguvu ya teknolojia yenye kasi ya kufanya uinjilisti bila mipaka.

Unganisha

Anzisha mawasiliano na ujenge uhusiano na hadhira yako.

Shirikisha

Hamasisha ushiriki wa moja kwa moja na mwingiliano kupitia ujumbe wako.

Badilisha

Wahimize hadhira yako kushiriki kikamilifu au kujitolea kwa ujumbe wa kiroho.

Kwa nini SDASMS?

SDASMS ni mfumo wa kutuma ujumbe wa maandishi (SMS) kwa idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja. Mfumo huu unatumika sana na makanisa, taasisi za makanisa (hospitali, shule na vyuo) na mashirika ya kiuinilisti kwa madhumuni mbali mbali kama vile kutangaza injili, kutoa taarifa muhimu kwa washiriki, watenda kazi wa kanisa, na mawasiliano mengine y amiradi ya kijamii. kwa kutumia huduma yetu, mtumiaji anaweza kutuma ujumbe mmoja ambao utawafikia walengwa wengi kwa haraka na kwa ufanisi.

Faida za mfumo wetu.

Ni Rahisi Kuutumia

Mfumo wetu wa Bulk SMS umeundwa kwa urahisi wa mtumiaji, kuhakikisha hata watu wasio na ujuzi wa teknolojia wanaweza kuitumia bila changamoto.

Usalama Hali ya Juu

Tunahakikisha usalama wa data na ujumbe wako kupitia mifumo ya kisasa ya ulinzi, hivyo taarifa zako zinabaki salama kila wakati.

Usimamizi wa Makundi (Groups)

Rahisisha usimamizi wa mawasiliano kwa kuunda makundi maalum, iwe ni kwa waumini, vikundi vya maombi, au washiriki wa huduma tofauti.

Ufuatiliaji wa Takwimu (Analytics)

Mfumo wetu unakupa ripoti za kina za takwimu kuhusu ujumbe uliotumwa, ikiwa ni pamoja na viwango vya kufikishwa na kusomwa kwa ujumbe.

Ujumbe wa Kibinafsi (Personalization)

Unaweza kuunda ujumbe wa kipekee unaolengwa kwa kila mpokeaji, kuongeza ufanisi wa mawasiliano yako.

Ratiba za Ujumbe (Schedules)

Ratibu ujumbe wako mapema kwa muda unaotaka ili kuhakikisha unafikia hadhira yako kwa wakati sahihi.

Zaidi ya Taasisi 5000 zinatumia huduma yetu.

Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.
Brand Name : Brand Short Description Type Here.

Maswali yanayoulizwa zaidi

Je, mfumo wenu unaruhusu mawasiliano ya pande mbili?

Ndiyo, tunatoa huduma ya mawasiliano ya pande mbili (two-way communication), lakini kwa maombi maalum. Huduma hii haiwezeshwi moja kwa moja na imetengwa kwa wateja maalum. Tafadhali wasiliana na kitengo chetu cha msaada kwa maelezo zaidi.

Je, naweza kuona hali ya ujumbe wangu uliotumwa?

Ndiyo, katika sehemu ya Ripoti kwenye dashibodi yako, utapata orodha ya ujumbe wote uliotumwa, iwe umefika au la. Hali ya ujumbe itaoneshwa, kama vile inasubiri (pending), namba isiyo sahihi (invalid number), au hitilafu nyingine yoyote.

Je, nitapata taarifa nikikaribia kumaliza salio la SMS?

Ndiyo, utapokea arifa moja kwa moja kupitia SMS au barua pepe pindi salio lako la SMS linapokaribia kuisha.

Ni muundo gani wa namba za simu unatakiwa kutumia unapoandaa orodha ya mawasiliano au kutuma ujumbe?

Andika namba ya simu bila alama ya “+” au “00” lakini ukiweka namba ya nchi mwanzoni. Kwa Tanzania, namba ya nchi ni +255, hivyo utaandika 255XXXXXXXXX. Iwapo unataka kutuma ujumbe kwa namba nyingi, tengenisha kila namba kwa koma (,).

Je, mnapatikana kwa msaada wa kiufundi?

Ndiyo, msaada wa kiufundi unapatikana kupitia barua pepe na simu. Tuna timu ya kiufundi inayopatikana masaa 24 kila siku. Unaweza pia kufungua tiketi ya msaada ili kuripoti tatizo kwa timu yetu ya kiufundi.

Je, kuna ada ya usajili au gharama za ziada?

Hapana. Tunatumia mfumo wa malipo ya kabla (prepay plan). Hakuna ada ya usajili wala gharama zozote za ziada.